Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amemtaka Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilolo kusimamia kikamilifu mradi wa ujenzi wa zahanati ya kata ya kilolo kwa kuzingatia muda wa mradi huo, usimamiza wa fedha na ubora wa viwango vinavyohitajika na Serikali. mwandishi wa matukio daima , Iringa
Hayo amezungumza jana alipotembelea mradi huo wa zahanati, na kuwataka viongozi kuongea ukweli wa hali inavyoendelea katika mradi huo wa zahanati na kutoendesha miradi kwa presha ili utekelezwaji uwe mzuri na katika kiwango chenye ubora .
''ni afadhari tukawa tunaongea ukweli kwamba kwa hali tunayoiona hapa kwenye huu mradi utachukua zaidi ya miezi saba na kama ukiisha ndani ya miezi mitano basi wewe upo kwenye sehemu salama kuliko kusema utamaliza mwezi wa tatu wakati ukienda nyumbani kulala unajua kuwa mradi ule mwezi wa tatu hapana matokeo yake sasa mtakuja hapa na presha ya kumaliza mradi, mtaweka mafundi mtawatia presha ni rahisi sana kupata vitu ambavyo vipo chini ya kiwango kwa sababu ya kukimbizana, hivyo tusijipe presha kwani mradi ni wa kwetu wenyewe hivyo tuutengenezee muda ambao tutautekeleza vizuri na kwa kiwango kinachotakiwa '', Amesema
Sendiga amemtaka mkurugenzi kutoandika changamoto ya taarifa ya kupanda bei ya vifaa kwani swala hilo linawekwa kijanja ili kujipatia manufaa kupitia mradi huo.
''kwenye taarifa hizi mnazoweka sipendi kuona kwenye changamoto hapo swala la upandaji wa vifaa, na ninaomba kwenye miradi inayokuja mkurugenzi kusiwepo na hilo la kupanda kwa bei, tumekuja kwa wananchi tumeanza kutafuta nguvu mapema kabla hatujaanza kujenga, Serikali imetuingizia milioni 400 kamili, tumetafuta fundi tumempata, ni nini kilikwamisha fundi kutoka na hesabu yake kamili kwamba ujenzi wa hili jengo litahitaji nondo tani nane akaenda kwa saplaya wa nondo kuuliza ni shilingi ngapi na akalipia nondo zote kwa wakati?, Sendiga
Hata hivyo amesema kuwa awamu hii ya sita ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu imejipanga na haitaki mchezo kwani watakuja kuonana wa moto kweli endapo wataendelea na ufujaji wa hela za miradi kiholela.
''mimi naomba miradi yote nitakayoendelea kuipitia swala la changamoto niendelee kuziona nyingine lakini sio changamoto ya upandaji wa bei ya vifaa labda tuwe tunapata fedha kwa mafungu mafungu hapo kutakuwa na changamoto kweli unaenda leo dukani una shilingi elfu 30 unanunua simenti halafu keshokutwa unaenda tena na hiyo hela ni rahisi kumkuta mwenye duka kashapandisha bei ya simenti, lakini kama una hela ya kutosha kwanini huendi kufanya booking ya simenti kama tani zako 30 unalipia zote kwa pamoja pale huwezi kukuta bei imepanda hata kama utakuwa unaenda kuchukua mojamoja maana ushazilipia zote tani 30 kwakweli sihitaji kuliona hilo swala''
Na kwa upande wa wanakijiji wamemshukuru Rais Samia pamoja na serikali yake kwa kuwajengea kituo cha afya ambacho kitawapunguzia changamoto wanazokutana nazo katika sekta ya afya.
''kituo cha afya kwetu ni muhimu sana kwa sababu mama anapokwenda kujifungua kama ni mtoto wa kiume anazaliwa kwa oparesheni analipia shilingi laki tatu na nusu na kwa mtoto wa kike analipa laki tatu mpaka laki mbili sasa hivi kwakweli kwa kituo hichi kinachojengwa sisi kwetu ni faraja kubwa na tunaamini tutaendelea kuishi kwa mafanikio makubwa hata kwa vizazi vijavyo, kwahiyo tunawiwa tuendelee kuwa na mahusiano na wakubwa wetu tuendelee kujenga ili upana wa maisha kwa sisi wananchi uendelee kuwepo'', amesema ndugu Lusungu Lufingu ambaye ni mwanakijiji wa kata hiyo.





0 Comments