Header Ads Widget

HABARI PICHA MAWAZIRI WAKIKAGUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI DODOMA

 MAWAZIRI WAIONGOZA KAMATI YA BUNGE KUKAGUA UJENZI JENGO LA MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI, JIJINI DODOMA, LEO, KAMATI YARIDHISHWA, YAPONGEZA KASI YA UJENZI WA JENGO HILO LINALOJENGWA NA SUMA JKT



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, wakati alipokuwa anawasili na Wajumbe wa Kamati yake kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Uhamiaji, jijini Dodoma, leo Oktoba 27, 2021, linalojengwa na SUMA JKT. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher KadioPicha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.




Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Tax (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, wakati alipokuwa anawasili katika mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Uhamiaji, jijini Dodoma, leo Oktoba 27, 2021, kabla ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, haijawasili katika eneo hilo kulikagua jengo hilo linalojengwa na SUMA JKT. 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Jeshi la Uhamiaji katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Tax, Waziri Simbachawene, na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika eneo la mradi wa ujenzi wa makao amkuu ya Uhamiaji jijini Dodoma, leo. Wapili Kushoto meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu, na wapili kulia ni Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Tax.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI