Bani Gantz anasema Israel inafaya kila linalowezekana kujilinda yenyewe
Februari 2, 2017, kundi la watu wasiojulikana walivunja milango ya ghala moja lililotelekezwa kwenye maeneo ya viwanda huko Tehran na kuvunja makufuli ya makasini 27 kwa muda wa chini ya saa 7 ili kuchukua maelfu ya ramani, hati na CD zilizo na taarifa za siri kuhusu mpango wa nyuklia wa Irani.
Miezi mitatu baada ya operesheni ya siri, nyaraka zilizoibiwa zilipatikana huko Tel Aviv, kilomita 2,000 kutoka Shurabad.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akionyesha vifuniko na masalia ya nyaraka na CD hizo na alisema ziliibiwa na mawakala wa Shirika la kijasusi la Mossad kutoka Tehran na kupelekwa Israeli.
Hata hivyo maafisa wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu iliyotuhumiwa waliita madai hayo kuwa uwongo na walighushi nyaraka, hata wakati wa uchaguzi wa urais, maafisa wa ngazi za juuu wa Irani akiwemo rais wa wakati huo Hassan Rouhani, alithibitisha wizi huo






0 Comments