Header Ads Widget

MBIO ZA SERENGETI SAFARI MARATHON 2026 ZAFANA, WASHIRIKI WAPONGEZWA




“Washiriki wote wa Mbio za Serengeti Safari Marathon ni washindi kila mmoja amechangia juhudi za uhifadhi wa mazingira, maliasili pamoja na kujenga afya bora kupitia michezo, bila kujali nafasi aliyopata".

Kauli hiyo imetolewa leo, Novemba 14, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Dkt. Khalfan Boniface Haule wakati akizungumza na washiriki wa Msimu wa Tisa wa mbio za Serengeti Safari Marathon zilizofanyika Geti la Ndabaka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wilaya ya Bunda mkoani Mara. 
Mbio hizo zimehusisha wakimbiaji wa kilomita 5, 10, 21 na 42 kutoka ndani na nje ya nchi. TANAPA imeendelea kutumia matukio ya kimichezo kama jukwaa muhimu la kutangaza vivutio vyake vya utalii vinavyopatikana nchini. Mbio hizo zimelenga kufungua fursa za kiuchumi wa buluu na kijani zitokanazo na vivutio vya utalii vinavyopatikana ukanda wa ziwa Victoria.














Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI