Mwili wa Mtangazaji Ebony Fm Edwin Bashiri kuzikwa leo saa 10 jioni makaburi ya familia Kibwabwa kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa,huku mwili wake kyagwa viwanja vya wazi vya KKKT Kibwabwa kuanzia saa 7 mchana na ibada itafanyika saa 3 asubuhi kanisa la Rc Parokia ya Mshindo.
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa chabeba gharama zote za mazishi ,Huku uongozi wa radio Ebony FM chini ya mkurugenzi wake Evarsto Mfugale wakijitolea kuandaa jukwaa na uwanja wa kuagia mwili pamoja na kaburi huku Radio Hatima Fm ya Arusha ikichangia sanduku lake.
Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa (MCC) Salim Abria Asas jana amefika kuhani msiba huo akiwa akiongozana na mwenyekiti CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin .



















































0 Comments