Mbungo, ambaye ni mwanzilishi wa kampuni za Toolboksi na Spana za nchini Tanzania alihudhuria sherehe za tuzo hizo zilizotolewa Oktoba 13, akiwaki mmoja wa vijana wa kitanzania waliohudhuria kati ya wanne waliopewa heshima hiyo kutokana na kuleta mabadiliko katika jamii.
Wengine walioshinda tuzo hizo kutoka Tanzania ni Editha Mshiu, Dkt Noely Mapunda, na Suleiman Salum Suleiman.Katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa Afrika Mashariki, Kenya pia ilikuwa na vijana wanne walioshinda tuzo hizo, Rwanda walipata washindi wawili na Uganda wakapata mshindi mmoja.
Tuzo hizo kwa vijana kati ya umri wa miaka 18 na 35, zilizotolewa na Queen Elizabeth II Commonwealth Trust zikiadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Malkia Elizabeth II na kuendeleza dhamira yake ya kusaidia vijana wanaoboresha maisha ya jamii zao.
Mbungo sambamba na washindi wengine kutoka mataifa mbalimbali pia walialikwa kuhudhuria mapokezi ya Mfalme na Malkia katika Kasri la St James’s jijini London, ambako alikutana na Mfalme Charles III na Malkia Camilla.
Mbungo anasema, kilichompa fursa ya kutambuliwa ni kutokana na jinsi alivyolenga makundi muhimu katika uchumi wa Tanzania ambapo kampuni zake zimekuwa zikisaidia mafundi na wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi.
“Nyuma ya heshima hiyo kuna kazi inayolenga mahitaji ya kawaida lakini muhimu kwa maisha ya mafundi,” anasema MbungoKupitia Kampuni yake ya Toolboksi, Mbungo anatumia teknolojia kuwaunganisha mafundi na kaya pamoja na biashara zinazohitaji huduma za ukarabati, matengenezo na ufungaji vifaa kwenye magari na vyombo vya moto.
Mbungo anasema jukwaa hilo la kiteknolojia linalenga kupanua fursa za kazi, kuendeleza ujuzi na kuwasaidia mafundi kujenga biashara zenye kipato endelevu.
Toolboksi iliyoanzishwa mwaka 2019, yenye mtandao wa mafundi zaidi ya 5,000 nchini Tanzania, inayowaunganisha mafundi wa sekta isiyo rasmi na fursa za kazi, kuanzia matengenezo madogo hadi miradi mikubwa, kwa lengo la kuongeza ajira na kipato.Ubunifu wake mwingine, ni katika Kampuni yenye huduma inaitwa ‘Spana’ ambalo ni jukwaa la teknolojia linalotumia Akili Unde (AI) kuwasaidia mafundi magari kutambua hitilafu, kufanya matengenezo kwa ufanisi na kukuza biashara zao, huku likiwasaidia wamiliki wa magari kupata huduma bora na kusimamia matengenezo ya magari yao






0 Comments