Header Ads Widget

MAGAZETINI LEO ALHAMISI .1.OKTOBA .2026:MGOMO WA MADEREVA WAACHA MAUMIVU, AHSANTENI WATANZANIA KWA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

 


 Uongozi wa Matukio wa Matukio Daima Media unatoa shukrani nyingi kwa wadau wake wote waliotenga muda wao kushiriki zoezi la upigaji kura za kuwania  tuzo za umahiri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini tuzo  Samia Kalamu Awards 2026 zinazoratibiwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA),kweli tumefurahishwa na ushirikiano mliotuonesha wakati wote wa zoezi hili toka pazia la upigaji kura lilipofunguliwa Mwezi Septemba 3-Septemba 30 majira ya saa 6:00 usiku zoezi lilipohitimishwa.

Tunawashukuru sana  kwa sasa tuendelee kusubiri majibu ya kura tulizopiga hadi hapo zoezi la utoaji tuzo litakapotangazwa na kati yetu wanne tulioingia fainali mmoja wetu kati ya Matukio Daima,Citizen,Simulizi za Sauti na Habari Leo ataibuka mshindi .

Pia tunaendelea kuwaomba ushirikiano wenu pindi mnapotuhitaji kwa ajili ya habari ,Matangazo na shughuli yoyote ya kijamii inayohitaji uwepo wetu msisite kuwasiliana nasi kwa namba 0754026299.

Imetolewa na mkurugenzi wa Matukio Daima Media Francis Godwin.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI