Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 7 katika kipimo cha Richter, limetokea eneo la Nagqu, eneo kubwa la milima kaskazini mashariki mwa Lhasa, mji mkuu wa Tibet, hii ni kulingana taarifa za vyombo vya habari vya eneo hilo
Takriban watu 16 wamefariki dunia, huku idadi ya waliojeruhiwa ikifikia 65, wakiwemo watu 11 waliojeruhiwa vibaya.
Mamia ya nyumba zimebomoka katika eneo hilo, barabara na huduma za umeme zimekatika katika maeneo yaliyoathiriwa.
Kulingana na shirika la habari la serikali ya China,Xinhua, takriban nyumba 339 zimebomoka, huku tathmini ya kiwango cha uharibifu ikiendelea.
Hili ndilo tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vingi zaidi katika eneo hilo tangu mwaka wa 2023, ambapo watu 120 walifariki kufuatia tetemeko la ukubwa wa 6.2 katika mkoa jirani wa Gansu nchini China.
Rais wa China, Xi Jinping, ametoa agizo la kuanzishwa kwa operesheni kubwa ya uokoaji kufuatia tetemeko hilo.
Tibet ni mojawapo ya maeneo yanayofuatiliwa kwa karibu zaidi nchini China. Upatikanaji wa taarifa katika eneo hilo unadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na serikali ya China, huku uandishi huru wa habari ukikabiliwa na vikwazo vingi.






0 Comments