Header Ads Widget

BURKINA FASO KUFANYA MAGEUZI YA HISTORIA INAYOFUNDISHWA SHULENI

Tangu kuanza kwa mwaka mpya wa masomo tarehe moja mwezi Oktoba 2026, mamlaka nchini Burkina Faso zimeanza mchakato wa “kuondoa athari za ukoloni” katika historia inayofundishwa kwenye mfumo wake wa elimu.

Burkina Faso, imekuwa ikiendeleza kampeni ya kupinga ubeberu na kutangaza mapinduzi ya maendeleo ya wananchi ambayo inahusisha mapinduzi katika jinsi historia ya nchi hiyo inavyokumbukwa na kufundishwa.

Katika taarifa yake ya tarehe 7 mwezi Septemba 2026, Waziri wa Elimu ya Sekondari na Mafunzo ya Ufundi Profesa Moumouni Zoungrana, alisema kuwa “ tutaondoa maelezo katika masomo ya historia na jiografia ambayo hayatutendei haki.”

Aliongezea kuwa “Hii ina maana kwamba hata katika vitabu vyetu, kuna taarifa za uongo zilizoandikwa kwa lengo la kutufanya tuonekane kama watu wasioweza kufikiri, kutudunisha na kupunguza uwezo wetu wa kufikiri. Na kwa muda mrefu tumekuwa tukikuza maadili haya na kuyapitisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine.”

Waziri huyo amesema ni wakati wa Burkina Faso kuwa na ujasiri wa kuvunja mfumo uliopo na kuujenga upya.

Profesa Zoungrana pia alitangaza kuwa mitaala ya elimu itafanyiwa marekebisho, ikiwemo masomo ya Historia, Jiografia na Elimu ya Uraia, akisema hatua hiyo inalenga kuondoa maelezo anayoyaona kuwa “hayana mantiki.”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI