Na Elamu nyaulingo (UoI), Matukio Daima Media
IRINGA, Wananchi wa Kata ya Mkwawa katika Jimbo la Iringa Mjini wameweka wazi kero zao mbele ya Mbunge wao, Mheshimiwa Fadhili Ngajilo, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Jumatano ya tarehe 16 mwezi wa tisa wakitaka utekelezaji wa haraka wa ahadi mbalimbali za maendeleo na kupongeza baadhi ya miradi ambayo imekamilika mpaka sasa
Wakizungumza na mbunge huyo wananchi walijumuisha Miongoni mwa kero zilizotajwa ni kuzimika kwa taa za barabarani kwa muda mrefu, hali ambayo imekuwa ikihatarisha usalama wao nyakati za usiku. Aidha, wananchi waliomba kuwekwa kwa matuta katika barabara ya kuelekea makaburini kutokana na magari kuendesha kwa kasi na kusababisha ajali.
Mmoja wa wakazi alisema taa za barabarani zimezimika kwa muda mrefu na kuomba Mbunge asaidie kuishinikiza Serikali kuzirejesha. Pia alieleza kuwa barabara ya kuelekea makaburini haina matuta, hivyo magari yanaendesha kwa kasi. “Kwa asilimia 80 ya vifo hapa vinatokana na ukosefu wa matuta. Tunaomba matuta yawekwe mara moja,” alisema Ngajiro.
Kwa upande mwingine, wananchi walieleza changamoto ya uchafuzi wa mazingira, wakisema gari la taka hufika mara moja kwa wiki na wakati mwingine halikusanyi taka katika maeneo yote. Mkazi wa Don Bosco, Joseph Chilangwa, alisema hali hiyo imewalazimu baadhi ya wananchi kutupa taka katika maeneo yasiyofaa kutokana na kukosekana kwa sehemu maalumu za kutupa taka. Pia aliomba hatua zichukuliwe kuboresha barabara ya eneo hilo ambayo imeharibika.
Kero nyingine iliyowasilishwa ni usalama. Mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo alisema wananchi wanaogopa kutoka nyakati za usiku kutokana na matukio ya uporaji wa fedha na simu. Alisema wananchi wamefika polisi mara kadhaa kutoa taarifa bila kupata suluhisho la kuridhisha, akimtaka Mbunge kuingilia kati suala hilo. Pia alieleza kuwa baadhi ya viongozi wa eneo hilo wamewahi kukumbana na vitendo vya uhalifu.
Katika mkutano huo, Kiongozi wa Bodaboda wa Kanda ya Mkwawa aliomba msaada wa kujengewa ofisi ya kituo chao, akisema eneo tayari limetengwa kwa ajili ya ujenzi. Alieleza kuwa vituo vingi vya bodaboda havina paa wala mazingira bora ya kufanyia shughuli zao, hivyo wakaomba msaada ili wapate makao makuu. Wananchi wengine pia walilalamikia uwepo wa mbwa wanaozunguka mitaani na kuwatisha wakazi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Fadhili Ngajilo, alisema dhamira yake si kuzungumza pekee bali kuhakikisha kero zinazowasilishwa na wananchi zinafanyiwa kazi. Alisema amepokea maombi ya wananchi na atayafanyia kazi kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine. Pia alisema amepokea wito kutoka Azam Sports na kutangaza mpango wa kujenga uwanja wa michezo kwa ajili ya vijana na wanawake.
Kuhusu Kivuko cha Rukosi, Mbunge huyo alisema wataalamu wanapaswa kutoa majibu ya wazi kuhusu namna ya kukamilisha mradi huo, huku akiahidi kuwa fedha zitaandikwa kwenye bajeti ili kazi hiyo ikamilike. Aliongeza kuwa kila ombi litakalowasilishwa na wananchi litawekwa kwenye ratiba ya Serikali ili liweze kupata majibu na hatua stahiki


.jpeg)





0 Comments