NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Serikali ya Tanzania imetangaza nafasi 150 za ufadhili wa masomo nchini Algeria kwa Watanzania waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwawezesha wanafunzi wenye ufaulu mzuri kupata fursa za kusoma nje ya nchi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda , amesema nafasi hizo zimetolewa na Serikali ya Algeria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, ambapo Serikali ya Algeria itagharamia ada za masomo ya wanafunzi hao, huku Serikali ya Tanzania kupitia Samia Scholarship ikigharamia gharama zao za maisha wakiwa nchini humo.
Prof Mkenda, akieleza kuhusu fursa hiyo, Serikali imesema imeamua kutumia utaratibu wa Samia Scholarship katika kuchagua wanafunzi watakaokwenda Algeria ili kuhakikisha nafasi hizo zinatolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi bila kujali uwezo wa familia zao kugharamia maisha wakiwa nje ya nchi.
Amesema kuwa, wanafunzi 150 watakaochaguliwa watatokana na kundi la wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao. Uteuzi utafuata mpangilio wa ufaulu, kuanzia aliyefanya vizuri zaidi.
"Iwapo mwanafunzi mmoja atakataa nafasi hiyo, nafasi yake itapewa anayefuata katika orodha ya ufaulu. Hivyo, Serikali itaendelea kushuka katika orodha hiyo hadi kupata wanafunzi 150 watakaokubali kwenda kusoma Algeria".amesema
Aidha, amesema majina ya wanafunzi hao 150 yanatarajiwa kuwekwa kwenye tovuti ya Wizara, huku wanafunzi watakaochaguliwa wakiwasiliana na Serikali kupitia simu kwa ajili ya kuthibitisha kama watakubali nafasi hizo.
Ameongeza kuwa, wanafunzi watakaokubali watawezeshwa katika maandalizi ya safari, ikiwamo kusaidiwa katika mchakato wa kupata pasipoti na maandalizi mengine muhimu kabla ya kwenda Algeria.
Amesema kuwa, wanafunzi hao wakiwa Algeria, wanafunzi hao watatumia mwaka mmoja katika maandalizi ya lugha ya Kifaransa, kwa kuwa masomo yao yatatolewa kwa lugha hiyo. Serikali imesema hatua hiyo pia itawasaidia wanafunzi kujiandaa vizuri kabla ya kuanza masomo yao.
Prof Mkenda, amesema fursa hiyo imeelezwa kuwa inalenga kuwafungulia milango Watanzania kutoka familia za kawaida, wakiwamo watoto wa wakulima na wafugaji, ambao licha ya kufanya vizuri katika masomo wanaweza kukosa uwezo wa kugharamia masomo na maisha nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, Serikali imesema nafasi nyingine 15 zitatangazwa baadaye kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi na Advanced Mathematics.
Awali, Serikali ilitoa nafasi 1,000 za Samia Scholarship kwa wanafunzi waliokuwa wamefanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi, huku nafasi hizo zikiwalenga wanafunzi watakaosomea maeneo kama hisabati, TEHAMA, sayansi asilia na tumizi, uhandisi pamoja na tiba.
Serikali imesema inaendelea kufanya mazungumzo na nchi nyingine rafiki zinazotoa fursa za ufadhili kwa Watanzania ili iweze kushiriki katika mchakato wa kuwachagua wanafunzi na kuwawezesha kupitia mpango wa Samia Scholarship.
Kwa utaratibu huo, Serikali inalenga kuhakikisha wanafunzi wanaofanya vizuri wanapata fursa ya kusoma katika vyuo vizuri nje ya nchi, huku ikisaidia gharama ambazo hazigharamiwi na nchi inayotoa scholarship.
BONYEZA LINK HII KISHA PIGA KURA ZOTE NNE BAADA YA KUFUNGUA NENDA SEHEMU
BONYEZA HAPA KUPIGA KURA ZOTE NNE
IMEANDIKWA PIGA KURA KISHA BONYEZA SEHEMU IMEANDIKWA NDIO
MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SKA2026 TUNAOMBA KURA YAKO WAWEZA KUPIGA KURA KIRAHISI KULIKO KUPITIA LINK HII







0 Comments