Na Matukio Daima Media, Morogoro
DHAHABU inayopatikana katika Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata mkoani Morogoro, imekuwa chanzo cha sintofahamu baada ya wachimbaji wadogo kudai kutonufaika ipasavyo na shughuli wanazofanya kwenye migodi hiyo, wakitaka Serikali kuweka utaratibu utakaohakikisha pande zote zinapata haki zao.
Kwa mujibu wa wachimbaji hao, changamoto kubwa ipo kwenye mgawanyo wa madini na gharama za uzalishaji, ambapo wanadai baada ya kugawana kinachopatikana bado hubeba gharama za mashine, vilipuzi, maji, kamba, roba na mahitaji mengine, huku wenye leseni wakidaiwa kutaka sehemu katika mgao wao.
Mmoja wa Wachimbaji Sadi Ahmad Amrani ameeleza wamekuwa wakizuiwa kusaga mawe yao katika mialo na karasha nyingine kwa kulazimishwa kusaga kwa mwenye Leseni, hali iliyoongeza changamoto, kwa kuwa mizigo hulazimika kusubiri muda mrefu hadi wenye leseni wamalize shughuli zao, hali wanayodai kufanya madini yao kukaa kwa muda mrefu kabla ya kuchakatwa na kukosa kipato.
Katika hoja nyingine, Mchimbaji Naomi Bless,kwaniaba ya wachimbaji hao ameomba wenye leseni kuheshimu mchango wao katika uchimbaji na kuwaacha kutumia maeneo mengine ya uchakataji, wakisema lengo lao si kugombana na wenye leseni bali kuwepo kwa makubaliano yanayowezesha kila upande kufanya shughuli zake na kunufaika.
Akasema kwa sasa wamechoka na tumechakaa, wakishindwa hata kukopesheka licha ya Kazi ngumu wanayoifanya ya kuhatarisha maisha yao kuingia kwenye mashimo, badala yake hata wakipaza sauti zao hutishiwa kufukuzwa kufanya kazi na Wenye leseni zao.
"Tunatumika kama tambala la deki, watu wananunua magari, wanapita nayo huku kwa mgongo wetu, sisi tunabaki maskini, tunaumia wao wanafanikiwa,bado wanataka mzigo Ukitoka tusagie kwao, Bado wamiliki na mgao wa wachimbaji licha ya kugharamia nzima za uendeshaji na Vifaa"Alisema Bless.
Hata hivyo, upande wa wenye leseni umepinga madai ya kuwanyanyasa au kuwazuia wachimbaji wadogo, ukieleza kuwa shughuli za migodini zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu, huku ukitaja kutokuwepo kwa makubaliano ya wazi kuhusu haki na majukumu ya kila upande kuwa sehemu ya changamoto.
Mmoja wa wakilishi wa wenye leseni ya Mosha,Roland August amesema ni kweli hawaruhusu mchanga au madini kuondoka maeneo yao kwamujibu wa Sheria, na kama Sheria inasema vinginevyo watakuwa tayari kupokea ushauri.
Mussa Kilakala Mkuu wa wilaya ya MorogoroNaye Tegemea Baraka alisema wachimbaji wadogo hawazuiwi kusaga madini yao nje ya maeneo yenye leseni na wamekuwa wakibeba kwapikipiki kupeleka kwenye mialo mingine kusaga, ingawa wananchi waliokuwepo walipinga maelezo hayo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala, na kudai kuwa mialo na karasha walizonazo hazitumiki kutokana na kuzuiwa na wenye leseni.
Baada ya kusikiliza pande hizo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala ameamua kuingilia kati kwa kuwataka wawakilishi wa wachimbaji wadogo na wenye leseni kufika ofisini kwake Jumatatu, huku wataalamu wa kada husika wakishirikishwa ili kupitia changamoto hizo na kutafuta suluhisho litakalowezesha shughuli za uchimbaji kuendelea kwa kuzingatia sheria na maslahi ya wahusika.
Mwisho














0 Comments