Header Ads Widget

RAIA 173 WA TANZANIA WAREJEA KUTOKA AFRIKA KUSINI

Takriban raia 173 wa Tanzania wamerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini.

Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake ulikuwa ume

toa mwito wa wale wanaotaka kurejea kwa hiari kufika katika ubalozi wa taifa hilo ulioko mjini Pretoria Afrika Kusini.

Kundi la kwanza liliwasili usiku wa kuamkia leo, huku kundi lingine likitarajiwa kuwasili hii leo.

Zoezi hilo litawahusisha Watanzania wasio na pasipoti, ambao muda wa kutumika wa pasipoti zao umekwisha au kupotea, pamoja na watoto waliozaliwa Afrika Kusini.

Watanzania wasio na pasipoti watapewa hati za dharura za kusafiria ili kuwawezesha kurejea nchini humo.

Uamuzi wa kuwarejesha Watanzania nchini unakuja wakati kumekuwa na maandamano ya kupinga wahamiaji nchini Afrika Kusini.

Mataifa kadhaa ya Afrika tayari yamewaondoa raia wao nchini humo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI