Header Ads Widget

PAPA LEO ATOA WITO WA KIMATAIFA KUIKABILI EBOLA


Papa Leo XIV ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kudhibiti mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC.

“Naishauri Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua zinazowahusisha pia jamii za wenyeji katika juhudi za kuzuia Ebola, ili kuokoa maisha ya watu wengi,” alisema Papa.Haya yanajiri baada ya Ebola kutajwa kuwa janga mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya DRC.

Mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, umefikia maambukizi 5,515 yaliyothibitishwa na kusababisha vifo vya watu 2,642.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali, visa vipya 51 vimeripotiwa katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini.

Mlipuko huo, uliotangazwa katikati ya Mei, ni wa 17 wa Ebola nchini humo na umetangazwa na Shirika la Afya Duniani, WHO, kuwa dharura ya afya ya umma yenye umuhimu wa kimataifa. Tahadhari hiyo pia inahusisha Uganda jirani.

Kwa mujibu wa serikali, kiwango cha vifo miongoni mwa walioambukizwa kimeongezeka kutoka takribani asilimia 20 mwanzoni mwa Juni hadi karibu asilimia 48 sasa, ikimaanisha kuwa karibu mtu mmoja kati ya wawili walioambukizwa wamefariki dunia

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI