Header Ads Widget

MAMA MARIAM MWINYI ATOA WITO WA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO, AIPA NGUVU SEKTA YA MWANI


Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, ametoa wito wa kuimarishwa kwa huduma za afya ya mama na mtoto, elimu ya afya pamoja na lishe bora, akisema hatua hizo ni muhimu katika kupunguza vifo na kujenga jamii yenye afya na ustawi.

Mama Mariam Mwinyi  ameyasema hayo leo, tarehe 31 Agosti 2026, wakati alipotembelea Taasisi ya WAJAMAMA Zanzibar, Mbweni, Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 31 Agosti, 2026 ambapo ameipongeza kwa juhudi za kutoa elimu na huduma zinazolenga kuboresha afya ya wanawake, wajawazito na watoto.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi ametembelea vikundi vya wakulima wa mwani Jambiani Kifumbwi Mkoa wa Kusini Unguja na kusisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya zao hilo badala ya kuliuza kama malighafi, ili kuongeza ajira, kipato na fursa za kiuchumi kwa wanawake na vijana.

Halikadhalika, amesema Zanzibar Maisha Bora Foundation itaendelea kushirikiana na wadau katika kuongeza uzalishaji, kuboresha mazingira ya kilimo cha mwani, kuongeza thamani ya bidhaa na kutafuta masoko yenye tija kwa wakulima, sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa Zanzibar.

















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI