Mpaka sasa hakuna mamlaka iliyothibitisha taarifa hiyo, ingawa BBC imezungumza na vyanzo vyake vya ndani serikalini vilivyothibitisha taarifa hiyo.
Vyombo vya habari vya ndani pia vimeripoti kuhusu taarifa hiyo ya kujiuzulu kwa Nchimbi.
Katika barua hiyo ambayo imechapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa Nchimbi, kiongozi huyo amesema amemwandikia Rais Samia Suluhu Hassan barua ya kujiuzulu.
Nchimbi ananukuliwa katika barua hiyo akisema kwamba uamuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa barua hiyo, auamuzi huo utaanza kutekelezwa Septemba 4, 2026.
Barua hiyo inasema wakati akiteuliwa kuwa Makamu wa Rais, alimuahidi Rais Samia kwamba angemsaidia kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu. Na kwamba alimwahidi pia Rais kwamba endapo siku moja angeona anahitaji Makamu mwingine wa Rais, angeachia nafasi hiyo.
"Siku yoyote akiona anahitaji Makamu mwingine wa Rais, nitaacha nafasi hii.", Inasema sehemu ya barua hiyo.
Kwenye barua hiyo, Nchimbi ananukuliwa kwamba amejiridhisha kuwa Rais Samia anatamani mabadiliko, hivyo ameamua kutimiza ahadi hiyo






0 Comments