Header Ads Widget

TAWI LA YANGA IRINGA MJINI KUPATA VIONGOZI JUNI 25



Tawi la Klabu ha jangwani, Yanga  tawi la Manispaaya Iringa linatarajia kufanya uchaguzi Juni 25.


Uchaguzi huo utafanyika kwenye ukumbi wa Lumilo hotel ukijumuisha wanachama hai wote.


Kwa mujibu wa Mjumbe wa kamati ya uchaguzi akimwakilisha Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hakimu Mwafongo alisema uchaguzi huo ni maandalizi ya mkutano mkuu wa Yanga utaofanyika baadaye.


Mjumbe Mwafongo alizitaja nafasi zinazowaniwa kuwa ni pamoja na uenyekiti wa tawi, makamu mwenyekiti, katibu, katibu msaidizi, mhazina na wajumbe wa tawi na mkutano mkuu.


Alisema maandalizi yote ya uchaguzi huo utakaotanguliwa na mkutano mkuu wa tawi yamekamilika ikiwemo kuchukua na kitudisha fomu kwa wagombea kumi waowania nafasi za uongozi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI