Header Ads Widget

MUHIMBILI YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UNYANYAPAA KUPITIA MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA

 


Watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiwemo wauguzi, wafanya usafi na wahudumu wa afya, wamepatiwa mafunzo maalum ya kupinga unyanyapaa mahali pa kazi kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma zenye utu, heshima na huruma kwa wagonjwa. 

Mafunzo hayo yamejikita katika kujenga mazingira ya kazi yanayokuza ushirikiano, upendo na kuheshimiana miongoni mwa watoa huduma pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya watoa huduma na wapokea huduma.

Mafunzo hayo yenye kaulimbiu “Unyanyapaa Haukubaliki” yameandaliwa kupitia ushirikiano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na mradi wa ETFA. 

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wamehamasishwa kutambua athari za unyanyapaa katika huduma za afya na kuchukua hatua za kujenga utamaduni unaothamini utu wa kila mtu, bila ubaguzi wala hukumu, ili kuhakikisha kila anayefika hospitalini anapata huduma katika mazingira salama, yenye ukarimu na yanayojali mahitaji yake.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI