Dodom:
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), ameipongeza Taasisi ya Utafiti Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ambapo watumishi wa taasisi hiyo wanatekeleza jukumu la kuhifadhi rasilimali ya wanyamapori kupitia tafiti.
Mhe.Kikwete ametoa pongezi hizo Juni 17,2026, alipotembelea banda la TAWIRI katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo alipata maelezo ikiwemo matumizi ya teknolojia katika kufatilia mienendo ya wanyamapori na mchango wa wadudu katika mfumo ikoloji.
Akibainisha ushiriki wa watumishi wa TAWIRI katika uhifadhi endelevu wa wanyamapori Mtafiti kutoka TAWIRI, Kipemba Ntiniwa amesema matumizi ya teknolojia mbalimbali ikiwemo mikanda ya visukuma mawimbi (GPS Colar) zinasaidia kuharakisha tafiti za wanyamapori na kupata takwimu za kisayansi kwa uhifadhi endelevu
Mtafiti Ntiniwa ameeleza tafiti wanazozifanya zinawagusa wanyamapori wakubwa na wadogo ambapo wadudu wanamchango mkubwa sana katika uhifadhi ikiwemo Huchavusha mimea kwa zaidi ya asilimia 80%, wadudu (Dung beetle) anasaidia utawanyaji na uoteshaji mbegu mwituni, umeng'enyaji virutubisho vya udongo hasa vinyesi vya wanyama (decomposition) na uongezaji mbole kwenye udongo (soil fertilization) na mzunguko wa chakulc (food chain)
Aidha, baada ya kukagua mabanda Mhe.Ridhiwani amesema Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ni jukwaa muhimu linalowawezesha wananchi kufahamu huduma
mbalimbali zinazotolewa na Serikali pamoja na namna ya kuzipata kwa urahisi.










0 Comments