Header Ads Widget

ARSENAL YATINGA FAINALI ULAYA BAADA YA MIAKA 20

 

Klabu ya Arsenal imefuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20, kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid, katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliopigwa katika uwanja wa Emirates.

Arsenal wamefuzu kwa jumla wa mabao 2-1 baad aya mchezo wa kwanza wa nusu fainali kule Madrid kutoka sare ya 1-1.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na Bukayo Saka katika kipindi cha kwanza, akimalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Atletico baada ya shuti la Leandro Trossard.

Hii ndiyo fainali yao ya pili katika historia ya michuano hiyo, ikifungwa 2-1 na Barcelona mwaka 2006.

Fainali ya mwaka huu itachezwa katika uwanja wa Puskás Aréna jijini Budapest, Hungary, Mei 30, ambapo Arsenal watakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Paris Saint-Germain na Bayern Munich.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI