Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE DKT NGWARU MAGHEMBE AWASILI NCHINI BRAZIL KWA ZIARA YA KIKAZI


Naibu waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt Ngwaru Maghembe (Mb.) amewasili nchini Brazil kwa ziara ya kikazi. Mhe. Naibu Waziri Dkt. Maghembe amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dr. John Stephen simbachawene katika Ofisi ya Ubalozi. Mhe Naibu waziri alipata nafasi ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali na Watumishi wa Ubalozi na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa kuvutia uwekezaji kutoka Brazili.

Katika ziara hiyo Mhe.Dkt Ngwaru Maghembe (Mb.) ataongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Mashauriano ya kisiasa kati ya Tanzania na Brazil. Mkutano huo unalenga kukuza uhusiano wa Kidiplomasia na Ushirikiano baina ya Tanzania na Brazili katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, Uwekezaji, Kilimo, Mifugo na Utalii




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI