Header Ads Widget

MADAM RITTA KUDHARAU CHOMBO CHA HABARI NI KUDHARAU MAMLAKA ZA SERIKALI



Na Matukio Daima Media .

IKIWA ni siku moja toka Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA)  kutangaza rasmi kusitisha ushirikiano wake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production, Rita Paulsen (Madam Rita) kufuatia kauli inayodaiwa kudhalilisha mwandishi wa Mike 360, Matukio Daima Media yapongeza msimamo huo.

Mkurugenzi wa Matukio Media  Francis Godwin ambae pia ni mwenyekiti wa Jumikita kanda ya nyanda za juu kusini amempongeza Mwenyekiti wa JUMIKITA kwa kuchukua hatua  ya kukemea lugha hiyo ya ovyo dhidi ya chombo cha habari  .

Kuwa ni hatua muhimu katika kulinda hadhi ya wanahabari na kuhakikisha taaluma hiyo inaheshimiwa na kila mdau.

"Sisi Matukio Daima Media tunaungana na JUMIKITA pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii kulaani vikali kauli ya Madam Rita, hii ni  dharau  isiyo na hekima inayoweza kuathiri taswira ya taaluma ya habari nchini anayedharau vyombo vya habari anapaswa kuogopwa  na kukimbiwa kama ukoma"

Hivi  kama  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa  leseni kwa chombo hicho na bodi ya ithibati imetoa  kitambulisho  kwa wanahabari wake kwanini Madam Ritta kashindwa   kuheshimu mamlaka hizo?

Kwani kauli za kudharau hazina nafasi katika kujenga jamii yenye kuheshimiana, Madam Ritta si tu amekikosea chombo hicho bali amewakosea watanzania wote wanaoheshimu Uhuru wa habari na kutegemea vyombo vya katika ujenzi upashaji habari .

Ni vizuri kuheshimiana na kila mmoja kuheshemu mwingine kama hivyo ndivyo ni wakati mzuri kwa Madam Ritta kuomba msamaha kwa kitendo hicho .

Awali akitoa msimamo wa JUMIKITA  Mwenyekiti Shaaban Matwebe alisema hatua hiyo imechukuliwa kulinda heshima ya taaluma ya uandishi wa habari, baada ya Madam Rita kudaiwa kumwambia mwandishi huyo kuwa hafanyi mahojiano na “media uchwara,” kabla ya kuondoka bila kutoa ushirikiano.

Matwebe alisema kuwa kauli hiyo ni ya kudhalilisha na haiendani na misingi ya heshima na usawa katika tasnia ya habari, akiongeza kuwa wanahabari wa mitandao ya kijamii wanafanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI