Waziri wa Maliasili na utalii nchini Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kukamilisha zoezi la kuwafunga tembo viongozi wa makundi mikanda ya visukuma mawimbi (GPS COLLARS) ili kufuatilia mienendo yao na kudhibiti Migongano kati yao na binadamu.
Dkt. Kijaji amesema hayo 03 Machi, 2026 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Viwanja vya Nanenane vilivyopo Njiro jijini Arusha.
Aidha, amesema kuimarika kwa Uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori kumechochea ukuaji wa sekta ya utalii nchini. “ idadi ya watalii imeongezeka kutoka 5,360,247 mwaka 2024 hadi watalii 5,935,561 mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 10.73” amefafanua Dkt. Kijaji
Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea na mikakati ya kuhakikisha wanyamapori wanakuwa salama na watu wanakuwa salama “Wanyamapori ni rasilimali muhimu katika uchumi wa nchi ambapo kupitia utalii kumekuwa na ongezeko la fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani Bilioni 3.9 hadi kufikia dola bilioni 4.4 sawa na ongezeko la asilimia 12.82.”
Akibainisha changamoto za sekta ya uhifadhi, amesema Kuongezeka kwa migongano baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu kunasababisha mahusiano hasi kati ya binadamu na wanyamapori “ nielekeze kufanyika tafiti za kimkakati ili kubaini mbinu mpya za kukabiliana na changamoto hii” amehimiza Dkt.Kijaji
Aidha, amesema udhibiti wa migongano unaendelea ambapo tembo 176 viongozi wa makundi wamefungwa mikanda Ya visukuma mawimbi ili kufuatilia mienendo yao na kuthibiti uharibifu. Pia Kwa mamba na viboko tayari
vizimba 18 vimejengwa maeneo mbalimbali nchini
















0 Comments