Header Ads Widget

TGNP YAWANOA WANAHABARI NJOMBE JUU YA MABADILIKO YA TABIANCHI NA USAWA WA KIJINSIA


Na Gabriel  Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika mkoa wa Njombe,Iringa na Mbeya wametajwa kuwa ndio waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi kutokana na asilimia zaidi ya 90 ya kundi hilo kujihusisha na shughuli za kilimo.

Hayo yamebainishwa na mwezeshaji wa mafunzo kutoka mtandao wa jinsia Tanzania TGNP Deogratius Temba wakati wa mafunzo kwa wanahabari mkoa wa Njombe kuhusu uandishi wa habari za jinsia na mbadiliko ya tabia nchi kupitia mradi wa Ustahimilivu wake,Dunia Yetu ambayo yamefanyika ukumbi wa green city Makambako,ambapo amesema licha ya kundi hilo kuathirika moja kwa moja na mabadiliko ya tabia nchi bado halijahusishwa kikamilifu kwenye ngazi za maamuzi hasa kutoa maoni yao juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Temba amesema jamii,serikali kuanzia ngazi za vijiji na wadau mbalimbali wanatakiwa kuwashirikisha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika jitihada za utatuzi wa changamoto za mabadiliko ya tabia nchi ili kuondoa changamoto zinazowakabili.

Mwezeshaji huyo amesema ikiwa waandishi wa habari wataandika habari kwa kuzingatia usawa na mabadiliko ya tabia nchi itasaidia kwa kiasi kukubwa kukabiliana na matukio ya ukatili kwa kuwa jamii itakuwa imejengewa uelewa kuhusu umhimu wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kushiriki kwenye ngazi za maamuzi.


Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Njombe ambao wameshiriki mafunzo hayo Sophia Issa,Patory Kadash,Zawia Haji,Stivin Ngole  wamesema watahakikisha wanafanyia kazi mafunzo hayo kwa kuandika habari kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ili kuondoa changamoto zinazowakabili wanawake na vijana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI