Katika kuadhimisha Kilele cha Siku ya Kimataifa ya wanawake Duniani Machi 08, 2026, wanawake wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) walikuwepo katika Mji wa Mikese, Mkoa wa Morogoro kuungana na wanawake wengine kutoka mashirika na taasisi kuadhimisha siku hiyo yenye kauli mbiu
"Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050” ikilenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.










0 Comments