Vikundi tisa wa sanaa vilivyokidhi ubora wa kisanii na ubunifu kupeleka ujumbe kwa jamii wamepokea ruzuku ya Feel Free Grant 2026 iliyotolewa na taasisi ya Nafasi Art Space ili waweze kuendeleza sekta ya sanaa nchini.
Mkurugenzi wa taasisi ya Nafasi Art Space Lilian Hipolity alisema jana jijini Dar es salaam kuwa, jumla ya shilingi 188,433,600 zimetolewa kusaidia utekelezaji wa miradi ya sanaa kuendeleza kazi na kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya sanaa nchini.
Alisema ruzuku hizo zinalenga kusaidia wasanii, wadau wa sanaa na taasisi za bunifu nchini na tayari watu na vikundi 32 kati yao asilimia 50 ni wanawake na asilimia 5o ni miradi ya nje ya jiji la Dar es salaam. Mpango unaoendeleza kutoa fursa kwa wasanii kupata rasilimali na uhuru wa kuendeleza miradi inayochochochea bunifu, majadiliano ya kitamaduni na uendelevu katika sekta ya sanaa.
Wasanii tisa waliopata ruzuku kati ya vikundi 24 vilivyochujwa ni John Kitime anayefanya sanaa ya nyimbo za asili za makabila, Victoria Mponda anafanya sanaa ya uchoraji wa ukutani wa wanawake wa kabila la wagogo kwa kuibadilisha kuwa miundo ya kidijitali na vitambaa. Mtandao wa wasanii wanawake Tanzania wanaofanya sanaa ya sarakasi kupitia mafunzo ya kitaaluma.
Kikundi cha Ayoub Bombwe wasanii 15 wanaojihusisha na sanaa za maonesho ya majukwani. Leila Ramadhani anayefanya sanaa ya uchunguzi wa sauti uhifadhi wa kumbukumbu kuipitiaa video na picha, kikundi cha Turakella Gyindo mradi unaochunguza desturi za usafi wa mwili, kikundi Nile Blues Project mradi wa kuhifadhi na kufufua ala za muziki wa asili wa Afrika kupitia mafunzo ya jamii kupitia elimu ya muziki na Fadhili Meta anayefanya sana za uzalishazji tamthilia ya jukwaa inayolenga viongozi wa jadi na vijana kuhusu mabadiliko ya kijamii na kitamaduni









0 Comments