Leo ni siku ya kipekee ya kukukumbuka na kukupongeza kwa mchango wako mkubwa katika jamii ya Iringa na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Maadhimisho ya siku yako ya kuzaliwa si tu sherehe binafsi, bali ni fursa kwa wana Iringa kutafakari na kuthamini matendo yako ya huruma, uzalendo na kujitolea kwa dhati kwa maendeleo ya watu bila kujali tofauti zao za kisiasa, kijamii au kiitikadi.
MCC ASAS, umeweka alama isiyofutika katika sekta ya afya ndani ya Mkoa wa Iringa. Umechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa wodi ya VIP katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, hatua iliyoboreshwa huduma kwa wananchi na kuongeza hadhi ya hospitali hiyo.
Vilevile, umewezesha ujenzi wa wodi ya watoto njiti, kituo cha damu salama pamoja na maboresho mengine muhimu katika sekta ya afya.
Haya yote si kwa manufaa yako binafsi, bali ni kwa faida ya jamii nzima ya wana Iringa.
Huduma hizi zimeokoa maisha ya wengi na kuleta matumaini mapya kwa familia nyingi ndani ya mkoa wetu.
Katika eneo la ustawi wa jamii na utawala, umejitolea kujenga jengo la ustawi wa jamii pamoja na kuboresha ofisi za Meya na Mbunge wa Iringa Mjini, na kuzifanya kuwa na hadhi inayostahili ofisi za uongozi wa umma.
Hatua hii imeimarisha utendaji kazi na kuongeza heshima ya taasisi hizi mbele ya wananchi.
Upande wa ujenzi wa chama, umeonyesha mapenzi ya dhati kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kujitolea kujenga ofisi za kisasa katika kata zote za Mkoa wa Iringa.
Hii ni hatua kubwa katika kuimarisha miundombinu ya chama na kuleta ufanisi katika shughuli za kisiasa na kijamii.
Katika sekta ya usalama barabarani, mchango wako umeonekana wazi. Ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, umechangia upatikanaji wa gari la wagonjwa na maboresho mbalimbali ndani ya kikosi cha usalama barabarani.
Juhudi hizi zimeongeza kasi ya uokoaji wa majeruhi wa ajali na kuimarisha usalama kwa watumiaji wa barabara.
Aidha, umeonyesha moyo wa kipekee wa kuwajali makundi maalum katika jamii. Umesaidia kuwajengea wazee makazi bora, kuwahudumia watoto yatima na kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji. Hii ni ishara ya uongozi unaogusa maisha ya watu moja kwa moja.
Kupitia kampuni za Asas Group, umefanikiwa kutoa ajira kwa vijana wengi, hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na kuongeza kipato kwa familia nyingi. Hii ni hatua muhimu katika kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Katika sekta ya elimu, umejitolea kusaidia ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mivinjeni, mradi uliokuwa ukisimamiwa na aliyekuwa Diwani wa Chadema, Marehemu Frank John Nyalusi. Kitendo hiki kinaonyesha kuwa maendeleo hayana chama; kinachotangulizwa ni ustawi wa wananchi.
Kwa hakika, MCC Salim ASAS, wewe ni kielelezo cha uongozi wa vitendo. Matendo yako yanaendelea kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya Iringa. Tunakuombea afya njema, maisha marefu na mafanikio zaidi ili uendelee kulitumikia taifa kwa moyo ule ule wa kujitolea.
Kila mwanadamu Mungu amemleta Duniani kwa makusudi maalum kwako MCC Asas makusudi ya Mungu kukuleta Duniani kila mmoja ni shahidi ameshuhudia kusudi la Mungu kupitia matendo yako .
Heri ya siku yako ya kuzaliwa. Mungu akubariki sana.







0 Comments