Header Ads Widget

MAGAZETINI LEO ALHAMISI FEB 26/2026

<

 

Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa wananchi kufuatia ongezeko la wagonjwa wa mafua makali ya Influenza na UVIKO-19 nchini. 

 Taarifa iliyotolewa leo jijini Dodoma na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, akieleza kuwa magonjwa hayo huenea kwa njia ya matone ya majimaji kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kupitia kukohoa, kupiga chafya au kuzungumza, pamoja na kugusa nyuso zilizochafuliwa. 

 Kwa mujibu wa Wizara, dalili za magonjwa hayo ni pamoja na homa kali, kikohozi, maumivu ya kichwa na mwili, mafua, kuwashwa koo na uchovu. 

 Takwimu za ufuatiliaji zinaonesha kuwa kila mwaka kuanzia mwezi Novemba hadi Aprili, kumekuwa na ongezeko la maambukizi hapa nchini na duniani kote, hali inayohitaji tahadhari zaidi kwa jamii. 

 Wizara imewahimiza wananchi kufunika pua na mdomo wanapokohoa au kupiga chafya, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono, na kuepuka misongamano isiyo ya lazima. 

Aidha, wananchi wametakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa na dalili au wanapokuwa katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu, pamoja na kuwahi vituo vya afya badala ya kujitibu au kutumia antibiotiki bila ushauri wa wataalamu. 

 Mbali na mafua makali na UVIKO-19, Wizara pia imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Homa ya Dengue kufuatia mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. 

Ugonjwa huo huenezwa na mbu aina ya Aedes ambaye huuma zaidi nyakati za asubuhi, mchana na jioni ambapo ametaja zake ni homa kali, maumivu ya kichwa na viungo, maumivu nyuma ya macho na uchovu. 

 Wananchi wametakiwa kutokomeza mazalia ya mbu kwa kuondoa maji yaliyotuama kwenye makopo, matairi na madimbwi, kuvaa nguo ndefu na kutumia dawa za kufukuza mbu. 

Pia, wametakiwa kuwahi vituo vya afya mara wanapoona dalili zinazofanana na Malaria au Dengue ili kupata uchunguzi na matibabu sahihi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI