Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAJASILIAMALI wadogo mkoani Kigoma wametakiwa kuijenga na kuitumia mitandao ya biashara (Business Networking) kwani ina mchango mkubwa kukuza shughuli zao za kiuchumi na biashara zao na kuzifanya kuwa zenye tija kubwa.
Katibu Tawala Msaidizi huduma za uchumi na mipango kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Deogratius Sangu alisema hayo akifungua mafunzo kwa wajasiliamali wadogo 50 yanayoratibiwa na Chemba ya wafanyabiashara wanawake (TWCC) mkoa Kigoma kupitia mradi wa Wezesha Binti unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL).
Sangu alisema kuwa mtandao wa biashara ambao unahusisha mahusiano ya biashara na wadau mbalimbali (Business Patrners Stake Holders) na Biashara mtandao (Business Digital Market) imewanyanyua wajasiliamali na wafanyabiashara wadogo kufanya biashara zao kwa ufanisi na kukuwa kibiashara na mtaji hivyo kuwataka wajasiliamali hao kuzingatia mafunzo hayo.
Mratibu wa Mradi wa wezesha binti kutoka Chemba ya wafanyabiashara Wanawake (TWCC) mkoa Kigoma, Tumaini Joseph
Akizungumzia mafunzo hayo Mratibu wa Mradi wa wezesha binti kutoka Chemba ya wafanyabiashara Wanawake (TWCC) mkoa Kigoma, Tumaini Joseph alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wajasiliamali wadogo namna ya kutengeneza mahusiano na wadau mbalimbali katika biashara ikiwemo mabenki na taasisi za fedha, mamlaka za usimamizi wa biashara, masoko na wafanyabiashara wengine ndani na nje ya nchii,
Baadhi ya wasichana waliohudhuria mafunzo hayo akiwemo Salha Saidi Mjaasilimali kutoka Kigoma Mjini alisema kuwa mafunzo hayo kwao ni jaambo kubwa na muhimu kwani yatawafundisha namna ya kutengeneza mahusiano na wadau mbalimbali ikiwemo benki, walimu wa kuwafundisha biashara zao lakini pia kuzifikia mamlaka mbalimbali kwa ajili ya kurasimisha biashara zao na kuzifanya kuwa za kitaifa na kimataifa.







0 Comments