Header Ads Widget

DC SAME ATOA SIKU 7 MIFUGO KUONDOLEWA SAME.



MATUKIO DAIMA MEDIA.

SAME. 

Serikali ya Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro, imetoa agizo kwa wafugaji wote walioingiza mifugo yao katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo bila kufuata taratibu na bila kuwa na vibali halali, kuiondoa mifugo hiyo ndani ya siku saba kuanzia leo. 

Agizo hilo limetolewa na Kasilda Mgeni, Mkuu wa Wilaya ya Same, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kitongoji cha Mbono, kijiji cha Kizungo, kata ya Vumari, wilayani humo.

Kauli hiyo imekuja kufuatia wananchi wa eneo hilo kuibua malalamiko kuhusu uwepo wa wafugaji na mifugo yao walioingia katika kijiji cha Kizungo wakitokea wilaya jirani kinyume na taratibu za uhamishaji wa mifugo.

 Wananchi hao wamedai kuwa eneo lao halina uwezo wa kuhimili ongezeko la mifugo zaidi kutokana na uhaba wa ardhi ya malisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI