Wakirejea athari za kukosekana kwa amani na utulivu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2025, wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimama imara na kuhakikisha amani, utulivu na usalama unarejea kote nchini na hivyo kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli zao.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti, wamezungumzia pia kuhusu umuhimu wa amani, Bi. Haddar Omari Salehe akisema amani ndio msingi wa maendeleo kote duniani, akisema inamsaidia kiuchumi kwani bila amani asingeweza kufanya biashara zake.
"Amani ndio kila kitu. Amani ikiwepo ndio unafuu wetu kama hivi kwasasa hivi tunamshukuru Mungu, tunatoka na tunapata riziki zetu. Amani iendelee hivi hivi na tunamuombea Mama Samia kila la kheri." Amesema Bi. Haddar.






0 Comments