Wananchi wa Jiji la Dar Es Salaam wameishukuru serikali kwa kuendelea kudumisha amani nchini pamoja na kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea kama kawaida, wakimuomba Mungu kuendelea kuwalinda na kuwapa utashi zaidi Viongozi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ili Tanzania iendelee kubakia salama na tulivu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bi. Ashura Hamis Mpoda, Mkazi wa Temeke Jijini Dar Es Salaam ameeleza kuwa amani na utulivu uliopo nchini umewezesha pia serikalo kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara.
"Sisi tunashukuru Mwenyenzi Mungu kwasasa Tanzania nzima ina amani na tupo salama. Tulitetereka baiashara zetu kwa changamoto zilizotokea lakini sasa tupo salama na mambo mengine yanaenda vizuri, tunatoka, watoto wanaenda shule na hata katika michezo. Mungu amlinde Rais wetu Samia ili aendelee kutufanyia mazuri." Amesema Bi. Mpoda.






0 Comments