Header Ads Widget

WAZIRI MKUU WA DENMARK AMUOMBA TRUMP KUKOMESHA 'VITISHO' DHIDI YA GREENLAND

 

Waziri mkuu wa Denmark amemwambia Donald Trump "kukomesha vitisho" vya kuichukua Greenland.

Mette Frederiksen anasema "vitisho vya Marekani kuichukua Greenland havina msingi wowote", na kuongeza: "Marekani haina haki ya kunyakua taifa lolote kati ya mataifa matatu katika ufalme wa Denmark."

Kauli yake inajiri baada ya Katie Miller - mke wa mmoja wa wasaidizi wa Trump, Stephen Miller - kuweka mtandaoni ramani ya Greenland yenye rangi za bendera ya Marekani sambamba na neno "SOON" kumaanisa ''HIVI KARIBUNI''.

Trump amerejelea mara kwa mara uwezekano wa Greenland kuwa sehemu ya Marekani.

Katika taarifa yake, iliyowekwa kwenye tovuti ya serikali ya Denmark, Frederiksen alisema alikuwa akisema na Marekani "moja kwa moja".

Alisema Denmark - "na hivyo Greenland" - ilikuwa mwanachama wa Nato na ina dhamana ya usalama ya muungano huo.

Denmark tayari ilikuwa na makubaliano ya ulinzi na Marekani ambayo yaliipa nafasi ya ufikiaji wa Greenland, alisema, na kuongeza kuwa Denmark imeimarisha uwekezaji usalama katika eneo la Arctic.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI