Header Ads Widget

TRUMP AMUONYA KIONGOZI MPYA WA VENEZUELA, MADURO AKITARAJIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

 


Rais wa Marekani Donald Trump amemuonya kiongozi mpya wa Venezuela Delcy Rodríguez kwamba anaweza "kukabiliwa vikali, pengine kuliko Maduro" ikiwa "hatafanya kilicho sahihi".

Kauli yake kwa jarida la Marekani la The Atlantic inakujawakati rais wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani Nicolás Maduro akitarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya New York leo Jumatatu.

Marekani inamshutumu Maduro, ambaye anashtakiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu wa silaha, kwa kuendesha serikali ya "magaidi wa mihadarati", madai ambayo anayakanusha.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesisitiza kuwa Marekani haiko vitani na Venezuela, baada ya mashambulizi ya anga mjini Caracas siku ya Jumamosi yaliyoishia Maduro na mke wake kuwekwa chini ya ulinzi na kusafirishwa hadi Marekani.

Baadhi ya wabunge wa chama cha Democratic wanasema operesheni hiyo ni "kitendo cha vita".

Katika mahojiano na The Atlantic Jumapili, Trump alisema kuhusu Rodríguez: "Ikiwa hatafanya kilicho sahihi, atalipa gharama kubwa sana, pengine kubwa kuliko Maduro."

Aliongeza kuwa kwa Wavenezuela, "Mabadiliko ya utawala, chochote unachotaka kukiita, ni bora kuliko ulichonacho sasa hivi. Haiwezi kuwa mbaya zaidi".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI