Header Ads Widget

WANAODHANIWA WAKATOLIKI 100 WAFIKA UBALOZI WA VATICAN WAKIMLALAMIKIA ASKOFU RUWA'ICHI, PADRI KITIMA


Zaidi ya waumini 100 wa Kanisa Katoliki leo wamefika katika Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania na kuwasilisha barua rasmi ya malalamiko dhidi ya Askofu Mkuu  Ruwa’ichi na Padri Charles Kitima.

Barua hiyo imekabidhiwa kwa njia ya utaratibu rasmi wa kidiplomasia, ikiwa na madai ya ukiukwaji wa maadili ya uongozi wa Kanisa, matumizi mabaya ya mamlaka ya kiroho na lugha zinazodaiwa kuwavunjia heshima waumini.

Hivi karibuni kumekuwa na msuguano ndani ya kanisa katoliki ambapo baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamejitokeza hadharani kupingana na misimamo ya viongozi wa kanisa hilo hususan kile kinachodaiwa viongozi hao kujikita kwenye mambo ya kisiasa hapa nchini badala ya kusimamia maadili ya kanisa kwa muujibu wa mafundisho ya vitabu vitakatifu





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI