Header Ads Widget

VIJANA TUNA DENI KWA RAIS SAMIA, "ANATUJALI NA KUTUPENDA"- KHALIFA


Watanzania wamempongeza na kumshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujasiri na uimaraka wake katika kulinda na kuitunza amani ya Tanzania kwa kusimama kidete katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo watanzania.

Pongezi hizo zimetolewa na Wakazi wa Mkoa wa Arusha akiwemo Bw. Hussein Khalifa, Mkazi wa Arusha Mjini, wakati akieleza kuhusu hatua mbalimbali za maendeleo zilizofikiwa kwenye Uongozi wa Rais Samia, wakati huu ambapo tunaelekea kuadhimisha siku 100 tangu kuapishwa kwake kuiongoza Tanzania kwa awamu ya pili.

"Mimi namsifu Amiri Jeshi wetu Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwanza kwenye amani, ambayo imeendelea kuwa tunu ya Tanzania kiasi cha kusifika  kote duniani na kuwa kimbilio la waliokosa makazi. Amekuwa Rais Jasiri pia na Rais wa kutumainiwa kiasi cha kuwa Mama yetu wa Taifa ambapo kwa ujasiri na ushupavu wake amani imeendelea kutawala nchini." Amesema Bw. Khalifa.

Akisisisita kuwa Vijana wanalo deni kwa Rais Samia  Khalifa amezungumzia pia mageuzi makubwa ya Vijana kupewa kipaumbele katika serikali ya Dkt. Samia kwa kuunda Wizara maalumu ya Vijana, akisema Rais Samia tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania, ndiye kiongozi pekee aliyetoa fursa ya Wizara kwa Vijana ili Vijana kuweza kutatuliwa changamoto zao kikamilifu chini ya Ofisi ya Rais.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI