Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kupitia Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii wa E.B.N Hunting Safari ilikabidhi viti mwendo viwili (2) pamoja na vifaa vya shule (madaftari na kalamu) kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Vifaa hivyo vilitolewa Januari 29,2026, katika Kongamano la Malezi, Vijana na Maadili lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida.







0 Comments