Header Ads Widget

TANZANIA YANADI VIVUTIO VYAKE MAONESHO YA FITUR NCHINI HISPANIA


Nchi ya Tanzania imeendelea kunadi vivutio vyake katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii FITUR( Feria Internacional de Turismo) yanayofanyika katika Kituo cha Maonesho cha IFEMA, jijini Madrid, Hispania. Maonesho hayo yameanza Leo rasmi tarehe 21 Januari 2026.

Maonesho ya FITUR yanayofanyika jijini Madrid, Hispania, yanalenga kuwa jukwaa kuu la kimataifa kwa sekta ya utalii duniani. Maonesho hayo yanajikita katika kukuza biashara za utalii, kuhamasisha ubunifu na matumizi ya teknolojia za kidijitali, pamoja na kuendeleza misingi ya utalii endelevu unaozingatia mazingira na jamii.

Aidha Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ni miongoni mwa taasisi linalotumia jukwaa hilo muhimu linalowakutanisha zaidi ya wadau wa sekta ya utalii mia tano (500) duniani kutangaza Hifadhi za Taifa za Tanzania katika soko la kimataifa, kuonesha vivutio vya kipekee ikiwemo wanyamapori, mandhari na utalii wa, pamoja na kuhamasisha fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana ndani ya hifadhi hizo.

Kupitia Maonesho ya FITUR, TANAPA inapata fursa ya kuimarisha mikakati ya utangazaji wa kimataifa, kujenga na kuimarisha ushirikiano na waendeshaji wa biashara ya utalii, wawekezaji na taasisi za kimataifa. Hatua hii inatarajiwa kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Hifadhi za Taifa za Tanzania, kuongeza mapato ya utalii na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo endelevu ya uhifadhi na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Kwa ujumla, ushiriki wa TANAPA katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii FITUR ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa, kuvutia masoko mapya ya watalii, na kuendeleza utalii endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI