| Mohamed Bajaber akishangilia goli lake katika mchezo wa kombe la NMB Mapinduzi Cup 2026 |
Na.Matukio Daima Media, Zanzibar.
MABINGWA mara nne wa Kombe la Mapinduzi, Simba SC, imepata alama tatu katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Muembe Makumbi City, Januari 3, 2026 uliochezwa majira ya saa mbili na robo usiku uwanja wa Amaan, Unguja, Zanzibar.
Katika mchezo huo wa kundi B kombe la NMB Mapinduzi, ulioanza kwa kasi kwa timu zote mbili, Simba ilipata ushindi wa goli moja lililofungwa na kipindi cha kwanza cha mchezo na mchezaji wake Mohamed Bajaber
Kwa ushindi, Simba SC imeweza kuongoza kundi B kwa alama tatu na goli moja, huku timu za Muembe Makumbi City ya Unguja na Fufuni ya Pemba, zikibakia na point moja kila moja baada ya mchezo wao wa kwanza waliokutana wakitoka sare ya 1-1.
Aidha, Simba inatarajiwa kushuka dimbani tena siku ya Jumatatu usiku Januari 5, 2026 kucheza na timu ya Fufuni, mchezo ambao utaamua timu moja kusonga mbele.
Mchezo huo Simba SC anahitaji sare ya aina yoyote ama ushindi kuingia hatua ya nusu fainali.
NMB Mapinduzi Cup 2026 inashirikisha timu 10, zikiwemo Yanga, Azam FC, Singida Black na TRA United na Simba SC za Tanzania Bara, Mlandege, KVZ, Fufuni FC na Muembe Makumbi City za Zanzibar, pamoja na URA ya Uganda inayoshiriki kama timu mwalikwa.
Michuano hiyo itakayofikia tamati Januari 13, 2026 siku moja baada ya Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ambapo inadhaminiwa na bank ya NMB, Just fit sports gear, Bank ya PBZ na wengine wengi.
| Baadhi ya mashabiki |
| Mchezaji bora wa mechi, Chamou Karaboue akiwa na hundi yake |
| Mchezaji wa Muembe Makumbi City,Yakoub Said Mohamed akiwa na tuzo ya mchezaji mwenye mchezo wa kiungwana (Fair play akiwa na hundi yake kutoka kwa mdhamini Mkuu wa kombe hilo, bank ya NMB. |
| Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker akizungumza mara baada ya mchezo wao. (Picha zote na Andrew Chale wa Matukio Daima Media). |





0 Comments