Na Josea Sinkala, Mbeya.
Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imepokea zaidi ya shilingi billion 40 kutoka Serikali kwa kuu na wadau kwa kipindi cha siku 100 za uongozi wa Serikali ya awamu ya sita kipindi cha pili kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yameel na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya bi. Erica Yegella, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya kuhusu mafanikio ya siku 100 za kwanza kwenye uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha pili tangu kufanyika Kwa uchaguzi Oktoba 29, 2025 na baadaye kutangazwa mshindi kwa nafasi ya kupitia urais.
Mkurugenzi Yegella wa Halmashauri ya Mbeya anaishukuru Serikali kuu kwa uidhinishaji mabilion ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji na miundombinu ya Barabara.
Pia amewashukuru wahisani mbalimbali kwa michango yao hata kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchochea maende ambapo amesema katika fedha hizo zimo pia za mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo baadhi zimetengewa kuhudumia elimu ya bila malipo, kumalizia vituo vya afya, shule na kulipa mishahara ya watumishi.
Kiongozi huyo mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya pia ameahidi Halmashauri yake kudumisha umoja na mshkamano miongoni mwa watumishi anaowaongoza, kushirikiana na waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa vijiji na wananchi ili kuhakikisha wanatekeleza mambo yanayotarajiwa na wananchi na kama ilivyoahidi CCM kwenye ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2025-2030.








0 Comments