Header Ads Widget

CAG AIPONGEZA TARURA kWA UJENZI WA MIUNDOMBINU



Dodoma

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ndg. Charles Kichere, leo Januari 9, 2026 ametembelea Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na kufanya kikao na Menejimenti ya Wakala huyo katika ukumbi wa ofisi za TARURA zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, CAG ameipongeza TARURA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini tangu kuanzishwa kwake. 

Amesema kuwa licha ya TARURA kuwa ni taasisi changa, mafanikio yake yanaonekana wazi kupitia ujenzi wa barabara na madaraja mengi yanayowarahisishia wananchi kupata huduma za kijamii na kiuchumi.

“TARURA haina miaka mingi tangu kuanzishwa kwake, lakini matokeo ya kazi zake yanaonekana. Barabara na madaraja mengi yamejengwa na wananchi wanaendelea kunufaika,” amesema CAG.

Aidha, amesema TARURA ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla, hivyo aliwataka waendelee kujenga miundombinu ya barabara kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yatamfanya mwananchi kufanya mazoezi ili kukabiliana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD).





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI