Header Ads Widget

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA RAI KWA VIJANA KUTAFUTA NJIA SAHIHI YA KUDAI HAKI

 





Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amewataka Vijana na Wanaharakati kutafuta njia sahihi ya kudai haki ikiwemo mazungumzo mezani akiwaasa kuwa vita na vurugu avijawahi kusaidia bali upelekea kupotea kwa amani huku akitolea mfano wa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo takribani ni zaidi ya miaka thelathini wanaitafuta amani ambayo imepotea.


Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Pili unaohusisha Pande Tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani UNHCR ambapo pia walitumia mkutano huo kusaini nyaraka zinazoelezea Mpango wa Urejeshwaji wa Wakimbizi Elfu Themanini na Sita na Mia Mbili Hamsini na Sita waliopo hapa nchini ambapo pia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Shabani Bihango na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani nchini Tanzania,Barbara Dotse waliishukuru Tanzania kwa kuhifadhi wakimbizi hao kwa muda unaozidi miaka thelathini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI