Header Ads Widget

MSD YASHIRIKI WIKI YA KIMATAIFA YA KUKABILIANA NA USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA UVIDA


Na. Matukio Daima Media,Dar es salaam.

BOHARI ya Dawa (MSD) katika kuunga juhudi mbalimbali za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini, inashiriki kongamano la Saba Afrika la wiki ya kukabiliana na Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (UVIDA) linalofanyika Jijini Dar es salaam Desemba 2-5, 2025.

Akizungumza katika kongamano hilo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano MSD, Bi. Etty Kusiluka, amesema wao kama wadau wa dawa Nchini, wanatoa elimu na kuonesha bidhaa mbalimbali za Afya kwa washiriki wanaotembelea banda lao.

Etty Kasiluka amebainisha kuwa wakiwa kama wazalishaji, wanunuzi, watunzaji na wasambazaji wa dawa ambayo ni bidhaa muhimu kwa ajili ya watu kongamano hilo ni muhimu kwao.



"Mkutano huu unazungumzia usugu wa dawa, tukiwa wadau wakubwa tupo hapa kuonesha bidhaa husika za dawa lakini pia  kukutana na wadau, kusikiliza mawasilisho yao.

Wataalamu wa MSD na Wafamasia wapo hapa wanashiriki kongamano na tutapata kujua changamoto zilizopo na hatua za kufuata." Amesema Etty Kasiluka.

Kupitia maonyesho hayo, MSD imepata fursa ya kueleza maboresho mbalimbali yanayoendelea chini ya taasisi hiyo,  kubadilishana mawazo na wadau wake, kupokea na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wateja wake, kupokea ushauri sambamba na kuonyesha baadhi ya bidhaa zake zilizoko ghalani.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI