Akisisitiza falsafa ya “Kasi, Kufikika na Teknolojia”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka amewataka Maafisa Maendeleo ya Vijana nchini kuendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili Vijana kwa njia za kimkakati na jumuishi kwa kuzingatia falsafa ya kasi, kufikika na matumizi ya teknolojia.
Aidha, Mhe. Nanauka amesema kufanya hivyo kutasaidia kuratibu na kutekeleza shughuli za maendeleo ya Vijana kwa ufanisi.
Amebainisha hayo wakati wa kufunga kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Miko na Halmashauri nchini kilichofanyika katikaUkumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo Disemba 18, 2025.
Katika kikao hicho mambo mbalimbali yameazimiwa yakilenga kuweka misingi ya utekelezaji wenye tija wa programu na afua za maendeleo ya Vijana, kuboresha uratibu pamoja na kuhakikisha rasilimali na fursa zinazotolewa na Serikali zinawanufaisha Vijana kijamii na kiuchumi.
Pia, kikao hicho kimeazimia kuendelea kuratibu majukwaa maalum ya Vijana kwa lengo la kusikiliza, kujadili na kutatua changamoto zao.
Vile vile, Mhe. Nanauka amebainisha azimio lingine kuwa Maafisa Maendeleo ya Vijana kutambua vituo atamizi vya Vijana vilivyopo katika maeneo yao.










0 Comments