Header Ads Widget

WAZIRI MKUU DKT.MWIGULU NCHEMBA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KAMPASI YA KILIMO YA UDSM LINDI

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameutaka uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kuhakikisha ujenzi wa kampasi ya kilimo mkoani Lindi unakuwa kitovu halisi cha wataalamu kilimo ili kuleta maendeleo ya sekta hiyo.

Dkt. Nchemba ametoa wito huo wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kampasi ya kilimo ya chuo cha Dar es salaam unaoendelea eneo la Ngongo  lililopo halmashauri ya manispaa ya Lindi mkoani Lindi.

Akizungumza Dkt.Nchemba amesema tunahitaji wataalamu na kulima kwa kisasa hatua itakayoleta mapinduzi ambayo yasingeweza kufikiwa bila elimu bora, utafiti wa kina na matumizi ya teknolojia ya kisasa.

Kwa upande wao chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM kupitia kwa mkuu wa chuo hicho Dkt.Jakaya Kikwete na makamu wa chuo Profesa William Anangisye wameeleza kuwa katika mwaka ujao wa masomo wa 2026/2027 kampasi ya ngongo itaanza kudahili wanafunzi.

Ujenzi wa kampasi hiyo ya kilimo unatekelezwa kupitia mkopo wa masharti nafuu wa benki ya Dunia chini ya mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) ambapo unagharimu shilingi bilioni 14.8 na hadi kufikia sasa umetekelezwa kwa asilimia 60.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI