Header Ads Widget

NCAA YAENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI KATIKA KATA ZILIZOPO WILAYANI NGORONGORO



 Na,Jusline Marco:Arusha

Uhusiano kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na jamii inayoishi ndani ya eneo la hifadhi umeendelea kuimarika kufuatia ziara za Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Bw. Abdul-Razaq Badru katika vijiji mbalimbali vilivyoko tarafa ya Ngorongoro ambapo Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Bw. Abdul-Razaq Badru amesema  Mamlaka inaendelea kutekeleza Miradi ya Maji katika kata za Endulen, Kakesio, Olbalbal na maeneo mengine katika Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.



Akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ngorongoro na Diwani wa Kata ya Endulen Elias Sakara Nagol, katika ziara yake iliyofanyika leo Desemba 20, 2025 wakati alipotembelea Kata ya Enduleni, wilayani Ngorongoro, Kamishna Badru  amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika usimamizi na utunzaji wa miradi hiyo ambayo inagharimu fedha za Serikali.




Aidha ameeleza lengo la ziara aliyoifanya katika Kata hiyo kuwa ni kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Uongozi wa hifadhi ya Ngorongoro na jamii, pamoja na kukagua maboresho ya miundombinu ya maji inayotumika kwa  matumizi ya wananchi, mifugo na wanyamapori.



Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Enduleni, Dkt. Elias Sakara Nagol, amempongeza Kamishna Badru na wasaidizi wake kwa kuendeleza uhusiano  ya karibu na jamii inayoishi ndani  kwa kuwatembelea mara kwa mara, kusikiliza kero zao na kushirikiana nao katika masuala mbalimbali ya kijamii na kuahidi kuwa wananchi wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa kutunza na kulinda hifadhi kupitia programu ya uhifadhi shirikishi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI