Header Ads Widget

TANZANIA IMEDHAMIRIA KULINDA AFYA, MAISHA YA WATU- DKT. NCHIMBI


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Tanzania imedhamiria kuhakikisha inalinda afya, maisha ya watu na mazingira kwa kutoa kipaumbele katika uimarishaji wa mfumo wa afya, kuwekeza katika utafiti wa kisayansi, na kuhimiza matumizi ya dawa kama yanavyokusudiwa kwa manufaa ya watanzania na dunia kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Maadhimisho ya Kanda ya Afrika ya Wiki ya Kimataifa ya Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa (WAAW2025), yanayofanyika Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam. 


Amesema hatua hizo ni katika kukabiliana na tishio linaloongezeka la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, ambapo pia ametoa wito kwa nchi za Afrika kujiunga katika mapambano hayo ya kimataifa kwa kuunga mkono juhudi za matumizi sahihi ya dawa hizo za kuokoa maisha, kwa kubadilishana ujuzi, kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha kwamba dawa za vimelea vya magonjwa zinabaki kuwa na nguvu kwa vizazi vijavyo.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa kupitia kubadilishana takwimu na uratibu wa utekelezaji wa sera katika mapambano dhidi usugu wa vimelea vya magonjwa. 

Amesema ushirikiano huo ni muhimu kwa kuwa maambukizo hayazuiliwi na mipaka ya kijiografia. Vilevile, Makamu wa Rais amesema uwekezaji katika uvumbuzi na utafiti ni muhimu kwa lengo la kuboresha zana mpya za uchunguzi, chanjo na matibabu mbadala ambayo yanaweza kupunguza utegemezi kwa dawa za asili za vimelea vya magonjwa na kuweza kudhibiti mabadiliko ya magonjwa yanayojitokeza kwa jamii moja moja. 

Pia, Makamu wa Rais ametaja umuhimu wa utoaji elimu kwa umma na ushirikishwaji wa jamii ili kuwezesha wananchi kufuata ushauri wa huduma ya afya, kukamilisha dawa zilizoagizwa, kuepuka matumizi mabaya ya dawa za vimelea vya magonjwa na dawa zinginezo na kuzingatia viwango vya kuzuia na kudhibiti maambukizi.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI