WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amewashukuru Watanzania kwa kuendelea kuonyesha utulivu, uzalendo na mshikamano katika kuilinda amani ya Tanzania wakati nchi ikijiandaa kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa ukaguzi wa hali ya ulinzi na usalama katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo, Waziri Simbachawene alisema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote nchini ili kuhakikisha sherehe hizo zinafanyika kwa usalama na utulivu.
Aliongeza kuwa ushirikiano unaoonyeshwa na wananchi ni uthibitisho wa dhamira ya pamoja ya kulinda amani na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana tangu kupatikana kwa Uhuru.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na vyombo vya habari wakati wa ukaguzi huo waliipongeza serikali kwa hatua inazoendelea kuchukua kuboresha usalama, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi katika kuimarisha amani ya nchi.






0 Comments