Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatano Disemba 10, 2025, amewapongeza wananchi kwa kuyakataa maandamano ya Disemba 09, 2025, akiwataka kujenga utamaduni wa kudumu wa kukataa maandamano na matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani Mkoani Arusha.
Mhe. Makalla amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kibiashara kwenye soko la Kilombero Jijini Arusha, akiahidi kuwa serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani Arusha vitaendelea kuhakikisha usalama na amani inakuwepo.
Mhe. Makalla kadhalika kando ya kuwahakikishia wananchi ulinzi na usalama muda wote, amehimiza pia umuhimu wa wananchi kujikita katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii, akionya na kutangaza utimamu wa Vyombo vya ulinzi na usalama katika kukabiliana na wote wanaopanga kufanya vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Arusha.








0 Comments