Header Ads Widget

MKURUGEZI WA KAMPUNI YA XMATION DIGITAL ATOA FULSA KWA VIJANA KUJIFUNZA UJUZI WA KIDIJITALI


Na Ashrack Miraji Matukio Daima 

Kampuni ya Xmation Digital imezindua rasmi ofisi zake mpya Jana katika hafla iliyoongozwa na Mkurugezi wa kampuni hiyo, Amon John, huku akitoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kujifunza ujuzi wa teknolojia na masuala ya kidijitali ili kuongeza uwezo wao wa kujiajiri.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Amon John aliwashukuru wageni waalikwa, waandishi wa habari na wadau mbalimbali kwa kujumuika katika tukio hilo muhimu, akisisitiza kuwa uzinduzi wa ofisi mpya ni hatua ya kimkakati katika kukuza ubunifu na mawasiliano ya kisasa nchini.

Alisema kuwa Xmation Digital imejikita katika utoaji wa suluhisho za kidijitali na ubunifu wa kuona, ikijumuisha uchapishaji wa majarida, vitabu, T-shirt zenye nembo, mabango na bidhaa nyingine nyingi zinazochangia kuboresha mawasiliano katika jamii.

Katika hotuba yake, Amon John alibainisha kuwa kampuni hiyo inalenga kuimarisha uwezo wa vijana kupitia mafunzo ya teknolojia, ili kuwawezesha kupata uelewa mpana na kujikita katika kujiajiri. Alisisitiza kuwa dunia ya sasa inaendeshwa na teknolojia, hivyo ni muhimu vijana kuitumia fursa hiyo kuongeza maarifa na kuandaa mustakabali bora wa kiuchumi.

“Kupitia ofisi hii mpya, tunapanua uwezo wetu wa kushirikiana na wadau wanaotafuta ubunifu, weledi na majibu yenye kuleta mabadiliko,” alisema

Amon John alitoa shukrani kwa washirika, familia, marafiki na wadau waliounga mkono safari ya Xmation Digital tangu mwanzo, huku akiipongeza jamii ya waandishi wa habari kwa mchango wao muhimu wa kusambaza taarifa sahihi kwa umma.

Uzinduzi huu umeelezwa kuwa mwanzo wa ukurasa mpya wa ukuaji na ubunifu, huku kampuni ikiahidi kuendelea kushirikiana na jamii, taasisi na vijana katika kukuza teknolojia na sekta ya uchapishaji nchini.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI